حَدَّثَنَا‭ ‬الْقَعْنَبِيُّ،‭ ‬عَنْ‭  ‬مَالِكٍ،‭ ‬عَنْ‭ ‬يَزِيدَ‭ ‬بْنِ‭ ‬عَبْدِ‭ ‬اللَّهِ‭ ‬بْنِ‭ ‬الْهَادِ،‭ ‬عَنْ‭ ‬مُحَمَّدِ‭  ‬بْنِ‭ ‬إِبْرَاهِيمَ،‭ ‬عَنْ‭ ‬أَبِي‭ ‬سَلَمَةَ‭ ‬بْنِ‭ ‬عَبْدِ‭ ‬الرَّحْمَنِ،‭ ‬عَنْ‭  ‬أَبِي‭ ‬هُرَيْرَةَ،‭ ‬قَالَ‭ ‬قَالَ‭ ‬رَسُولُ‭ ‬اللَّهِ‭ ‬صلى‭ ‬الله‭ ‬عليه‭ ‬وسلم‭ ‬‏”‏‭  ‬خَيْرُ‭ ‬يَوْمٍ‭ ‬طَلَعَتْ‭ ‬فِيهِ‭ ‬الشَّمْسُ‭ ‬يَوْمُ‭ ‬الْجُمُعَةِ‭ ‬فِيهِ‭ ‬خُلِقَ‭  ‬آدَمُ‭ ‬وَفِيهِ‭ ‬أُهْبِطَ‭ ‬وَفِيهِ‭ ‬تِيبَ‭ ‬عَلَيْهِ

Siku bora lipandapo (linapochomoza) jua ni (siku) ya ijumaa. Katika siku hii, Mwenyezi Mungu (ndiyo siku) aliyomuumba Adamu (a.s), na katika siku hii alitubu kwa Mwenyezi Mungu. (Sunan Abu-Dawud, Kitab Al-Salat hadith na. 1046).

Mtume Muhammad (s.a.w) anatujulisha mambo mawili muhimu yanayofanya siku ya ijumaa iwe bora miongoni mwa siku za juma. Kwanza ni kwamba, hii siku ya Ijumaa ndiyo aliyoumbwa Adamu. Pili ni kwamba siku hii ya ijumaa, baada ya Adamu kumkosea Mwenyezi Mungu aliomba msamaha na toba yake ikapokelewa. Tunahitaji kuyaangalia mambo haya mawili kwa kina zaidi ndani ya vitabu vitakatifu vya Mwenyezi Mungu.

 

Kuumbwa kwa Adamu katika siku ya Ijumaa

 

Tutatumia Biblia na Qur’an ili kubainisha kwamba Adamu aliumbwa katika siku ya ijumaa. Jambo la kwaza tuangalie, je hii siku ya ijumaa katika Biblia inaitwa siku gani?

Kwa mujibu wa lugha ya Kiarabu na Kiebrania ambazo ndizo lugha za Vitabu Vitakatifu, Biblia (Agano la Kale) na Qur’an, siku zinajulikana kwa majina kama ifuatavyo katika jedwali hapa chini.

KIEBRANIA

KIARABU

KALENDA

KISWAHILI

BIBLIA

(Agano la Kale)

Yom 

Rishon

Yaum Al-ahad

Siku ya kwaza

Juma Pili

Siku ya Kwanza ya Juma

Yom 

Sheni

Yaum Al-Ithnayn

Siku ya pili

Juma Tatu

Siku ya Pili ya Juma

Yom 

Shilishi

Yaum Al-Thulathau

Siku ya tatu

Juma Nne

Siku ya Tatu ya Juma

Yom 

    Revi’i

Yaum Ar-Rabiu’

Siku ya nne

Juma Tano

Siku ya nne ya Juma

Yom 

Hamishi

Yaum Al-Khaamisu

Siku ya tano

Al Hamisi

Siku ya Tano ya Juma

Yom 

Shishi

Yaum Al-Jumua’t

Siku ya kusanyiko

Ijumaa

Siku ya Sita 

(Siku ya Maandalio 

ya Sabato)

Yom 

Shabbat

Yaum As Sabt

Siku ya sabato

Juma mosi

Siku ya Saba

 

 

Kutokana na jedwali hili tunagundua kwamba siku za juma katika lugha za asili zilizotumika kuandika vitabu vitakatifu zinaitwa kutokana na mfuatano wa namba, yaani siku ya kwanza, ya pili, ya tatu n.k. Siku mbili tu ndizo zimepewa majina tofauti na namba. Siku ya sita katika kiarabu inaitwa siku ya jumuiko (kukutanika) na siku ya saba kwa kiarabu na kiebrania inaitwa siku ya Sabato (siku ya mapumziko). Mabadiliko ya majina haya ni kutokana na sababu za kidini kama tutakavyoona hapo mbele.

Hivyo tunaona kwamba siku ya ijumaa kwa jina lingine ni siku ya sita. Sasa tuangalie uumbaji wa Adamu katika Biblia. Je, Biblia inasema Adam aliumbwa siku ya ngapi? Tunasoma katika kitabu cha Mwanzo 1:26-31;

“Mungu akasema, na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimuumba mwanamme na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi…Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita”.

Kama tulivyoona katika hadithi ya mtume Muhammad (s.a.w) kuwa Adamu aliumbwa katika siku ya ijumaa, na pia tumeona kwamba siku hii ya ijumaa kwa lugha ya Biblia inaitwa siku ya sita. Hivyo ni wazi kwamba hadithi hii ya mtume ni sahihi kabisa ya kuwa Adamu aliumbwa siku ya ijumaa, ingawa Qur’an haijaeleza kuwa Adamu aliumbwa siku ya ngapi.

Mtume Muhammad (s.a.w) pia anakubaliana na Biblia kwamba Adamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu na kwa sura ya Mungu kama tulivyosoma hapo juu katika Biblia. Tunasoma hadithi ya mtume katika Sahihi Bukhari hadithi na. 6227;

حَدَّثَنَا‭  ‬يَحْيَى‭ ‬بْنُ‭ ‬جَعْفَرٍ،‭ ‬حَدَّثَنَا‭ ‬عَبْدُ‭ ‬الرَّزَّاقِ،‭ ‬عَنْ‭ ‬مَعْمَرٍ،‭  ‬عَنْ‭ ‬هَمَّامٍ،‭ ‬عَنْ‭ ‬أَبِي‭ ‬هُرَيْرَةَ،‭ ‬عَنِ‭ ‬النَّبِيِّ‭ ‬صلى‭ ‬الله‭ ‬عليه‭ ‬وسلم‭  ‬قَالَ‭ ‬‏”‏‭ ‬خَلَقَ‭ ‬اللَّهُ‭ ‬آدَمَ‭ ‬عَلَى‭  ‬صُورَتِهِ،‭ ‬طُولُهُ‭ ‬سِتُّونَ‭ ‬ذِرَاعًا،‭ ‬فَلَمَّا‭ ‬خَلَقَهُ‭ ‬قَالَ‭ ‬اذْهَبْ‭  ‬فَسَلِّمْ‭ ‬عَلَى‭ ‬أُولَئِكَ‭ ‬النَّفَرِ‭ ‬مِنَ‭ ‬الْمَلاَئِكَةِ‭ ‬جُلُوسٌ،‭  ‬فَاسْتَمِعْ‭ ‬مَا‭ ‬يُحَيُّونَكَ،‭ ‬فَإِنَّهَا‭ ‬تَحِيَّتُكَ‭ ‬وَتَحِيَّةُ‭  ‬ذُرِّيَّتِكَ‏‭.‬‏

 

“Hadithi ya Abu Huraira: kutoka kwa mtume (s.a.w) amesema, Mwenyezi Mungu alimuumba Adamu kwa sura yake (mfano wake) na urefu wake ulikuwa dhiraa sitini (kama mita 30 hivi). Alipokwisha kumuumba akamwambia, enenda ukawasalimie kundi lile la malaika waliokaa hapo na usikie jinsi watakavyokuitikia. Kwa kuwa hii ndiyo itakuwa salamu yako na ya vizazi vyako…” (Tazama pia Sahihi Muslimu hadith namba 2841).

حَدَّثَنَا‭ ‬نَصْرُ‭ ‬بْنُ‭ ‬عَلِيٍّ‭ ‬الْجَهْضَمِيُّ،‭ ‬حَدَّثَنِي‭ ‬أَبِي،‭ ‬حَدَّثَنَا‭ ‬الْمُثَنَّى،‭ ‬ح‭ ‬وَحَدَّثَنِي‭ ‬مُحَمَّدُ‭ ‬بْنُ،‭  ‬حَاتِمٍ‭ ‬حَدَّثَنَا‭ ‬عَبْدُ‭ ‬الرَّحْمَنِ‭ ‬بْنُ‭ ‬مَهْدِيٍّ،‭ ‬عَنِ‭ ‬الْمُثَنَّى‭ ‬بْنِ‭ ‬سَعِيدٍ،‭ ‬عَنْ‭ ‬قَتَادَةَ،‭ ‬عَنْ‭ ‬أَبِي‭ ‬أَيُّوبَ،‭ ‬عَنْ‭   ‬أَبِي‭ ‬هُرَيْرَةَ،‭ ‬قَالَ‭ ‬قَالَ‭ ‬رَسُولُ‭ ‬اللَّهِ‭ ‬صلى‭ ‬الله‭ ‬عليه‭ ‬وسلم‭ ‬وَفِي‭ ‬حَدِيثِ‭ ‬ابْنِ‭ ‬حَاتِمٍ‭ ‬عَنِ‭ ‬النَّبِيِّ‭  ‬صلى‭ ‬الله‭ ‬عليه‭ ‬وسلم‭ ‬قَالَ‭ ‬‏”‏‭ ‬إِذَا‭ ‬قَاتَلَ‭ ‬أَحَدُكُمْ‭ ‬أَخَاهُ‭ ‬فَلْيَجْتَنِبِ‭ ‬الْوَجْهَ‭ ‬فَإِنَّ‭ ‬اللَّهَ‭ ‬خَلَقَ‭ ‬آدَمَ‭  ‬عَلَى‭ ‬صُورَتِهِ

 

“Hadithi ya Abu Huraira, amesema: (Na katika hadithi ya ibn Haatim kutoka kwa mtume s.a.w) amesema mtume s.a.w, ikiwa mmoja wenu atapigana na ndugu yake, basi aepuke kumpiga usoni, kwa sababu, Mwenyezi Mungu alimuumba kwa mfano wake” (Sahihi Muslimu 2612).

Ni wazi kwamba Qur’an haielezi ni katika siku gani Adamu aliumbwa, lakini umma wa waislam unakubaliana na hadithi ya mtume kwamba aliumbwa siku ya ijumaa. Ni sahihi pia kukubaliana na mtume katika jambo la pili kwamba Adamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu. Hii ni kwa sababu tayari Qur’an imekwisha kusema kwamba;

وَمَا‭ ‬يَنطِقُ‭ ‬عَنِ‭ ‬الْهَوَىٰ‭ ‬إِنْ‭ ‬هُوَ‭ ‬إِلَّا‭ ‬وَحْيٌ‭ ‬يُوحَىٰ

 

“Wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake) (Sura ya 53:4).

Ibn Kathir anasherehesha aya hii katika tafsir yake akimunukuu swahaba wa mtume Abdhullah bin Amr akisema;

حدثنا‭ ‬يحيى‭ ‬بن‭ ‬سعيد‭ ‬عن‭ ‬عبيد‭ ‬الله‭ ‬بن‭ ‬الأخنس‭ ‬أخبرنا‭ ‬الوليد‭ ‬بن‭ ‬عبد‭ ‬الله‭ ‬عن‭ ‬يوسف‭ ‬بن‭ ‬ماهك‭ ‬عن‭ ‬عبد‭ ‬الله‭ ‬بن‭ ‬عمرو‭ ‬وقال‭ ‬كنت‭ ‬أكتب‭ ‬كل‭ ‬شيء‭ ‬أسمعه‭ ‬من‭ ‬رسول‭ ‬الله‭ ‬صلى‭ ‬الله‭ ‬عليه‭ ‬وسلم‭ ‬أريد‭ ‬حفظه‭ ‬فنهتني‭ ‬قريش‭ ‬فقالوا‭ ‬إنك‭ ‬تكتب‭ ‬كل‭ ‬شيء‭ ‬تسمعه‭ ‬من‭ ‬رسول‭ ‬الله‭ ‬صلى‭ ‬الله‭ ‬عليه‭ ‬وسلم‭ ‬ورسول‭ ‬الله‭ ‬صلى‭ ‬الله‭ ‬عليه‭ ‬وسلم‭ ‬بشر‭ ‬يتكلم‭ ‬في‭ ‬الغضب‭ ‬فأمسكت‭ ‬عن‭ ‬الكتاب‭ ‬فذكرت‭ ‬ذلك‭ ‬لرسول‭ ‬الله‭ ‬صلى‭ ‬الله‭ ‬عليه‭ ‬وسلم‭ ‬فقال‭ ‬اكتب‭ ‬فوالذي‭ ‬نفسي‭ ‬بيده‭ ‬ما‭ ‬خرج‭ ‬مني‭ ‬إلا‭ ‬الحق‭ ‬ورواه‭ ‬أبو‭ ‬داود

 

“Hadithi ya Abdullah bin Amr amesema: Nilikuwa nikiandika kila kitu nilichokisikia kutoka kwa mtume (s.a.w) ambacho nilipenda kukihifadhi.  Makuraishi wakanikataza wakisema, ‘wewe waandika kila kitu kutoka kwa mtume (s.a.w)? Yeye ni mtu anaweza kuongea kwa ghadhabu yake, basi nikaacha kuandika. Nikamweleza mtume (s.a.w) juu ya jambo hili. Mtume akasema, ‘andika, maana kwa yeye ambaye nafsi yangu i mikononi mwake, hakuna kinachotoka kwangu isipokuwa ni kweli…”.

Na Katika Hadithi ya Abu Huraira amesema 

حدثنا‭ ‬يونس‭ ‬حدثنا‭ ‬ليث‭ ‬عن‭ ‬محمد‭ ‬عن‭ ‬سعيد‭ ‬بن‭ ‬أبي‭ ‬سعيد‭ ‬عن‭ ‬أبي‭ ‬هريرة‭ ‬عن‭ ‬رسول‭ ‬الله‭ ‬صلى‭ ‬الله‭ ‬عليه‭ ‬وسلم‭ ‬أنه‭ ‬قال‭ ‬لا‭ ‬أقول‭ ‬إلا‭ ‬حقا‭ ‬قال‭ ‬بعض‭ ‬أصحابه‭ ‬فإنك‭ ‬تداعبنا‭ ‬يا‭ ‬رسول‭ ‬الله‭ ‬قال‭ ‬إني‭ ‬لا‭ ‬أقول‭ ‬إلا‭ ‬حق

 

“Kutoka kwa mtume (s.a.w) amesema: sisemi ila yaliyo ya kweli…” (Tazama Tafsir ibn Kathir juu ya sura ya 53:4).

Hivyo basi ikiwa Qur’an inasema kwamba mtume hasemi kwa matamanio yake, na mtume mwenyewe anasema yote anayoyasema ni ya kweli, basi ni kweli kwamba kama alivyosema mtume, Adamu aliumbwa kwa mfano na sura ya Mwenyezi Mungu. Hii sasa ni sawa kabisa na Biblia iliposema, “Mungu akasema, na tufanye mtu kwa mfano wetu…kwa mfano wa Mungu, aliwaumba mwanamume na mwanamke”.

Vitabu vitakatifu vinatuambia kwamba, Mungu hafanani na chochote, wala hawezi kufananishwa na kitu.

وَلَمْ‭ ‬يَكُن‭ ‬لَّهُ‭ ‬كُفُوًا‭ ‬أَحَدٌ

 

“Wala hana anayefanana naye hata mmoja” (Sura ya 112:4).

“Hapana anayefanana na Mungu..” (Kumbukumbu la torati 33:26).

Mungu mwenyewe anauliza katika kitabu cha Isaya 46:5;

“Mtanifananisha na nani, na kunisawazisha naye, na kunilinganisha naye, ili tuwe sawasawa?”

Wakati huo huo Mwenyezi Mungu mwenyewe amesema anaumba mtu kwa mfano wake, na kauli hiyo inakubaliwa na mtume kwamba Mungu alimuumba Adamu kwa mfano wake. Hivyo ni wazi kwamba Mungu hakatai kufanana na kitu katika baadhi ya sifa isipokuwa katika kuabudiwa, kusujudiwa, ni yeye tu ndiye anayesitahiki kuabudiwa na kupewa heshima na siyo kitu kingine chochote. Kwa mfano, yeye mwenyewe amekataa kupigia magoti, au kusujudia kiumbe kingine akisema;

 “Usiwe na miungu wengine ila mimi…usijifanyie sanamu ya kuchonga wala mfano wa kitu chochote…usikisujudie” (Kutoka 20:1-4). 

وَاعْبُدُوا‭ ‬اللَّهَ‭ ‬وَلَا‭ ‬تُشْرِكُوا‭ ‬بِهِ‭ ‬شَيْئًا‭ ‬وَبِالْوَالِدَيْنِ‭ ‬إِحْسَانًا‭ ‬وَبِذِي‭ ‬الْقُرْبَىٰ‭ ‬وَالْيَتَامَىٰ‭ ‬وَالْمَسَاكِينِ‭ ‬وَالْجَارِ‭ ‬ذِي‭ ‬الْقُرْبَىٰ‭ ‬وَالْجَارِ‭ ‬الْجُنُبِ‭ ‬وَالصَّاحِبِ‭ ‬بِالْجَنبِ‭ ‬وَابْنِ‭ ‬السَّبِيلِ‭ ‬وَمَا‭ ‬مَلَكَتْ‭ ‬أَيْمَانُكُمْ‭ ‬إِنَّ‭ ‬اللَّهَ‭ ‬لَا‭ ‬يُحِبُّ‭ ‬مَن‭ ‬كَانَ‭ ‬مُخْتَالًا‭ ‬فَخُورًا

 

“Muabuduni Mwenyezi Mungu, wala msimshirikishe na chochote…” (Qur’an sura ya 4:36). 

Hivyo kwa mujibu wa vitabu vitakatifu, Biblia, Qur’an na Hadithi za mtume s.a.w, Adamu aliumbwa siku ya ijumaa na aliumbwa kwa mfano wa Mwenyezi Mungu. Basi siku hii lazima iwe bora na yenye heshima sana kwa sababu ni siku ambayo wazazi wetu Adamu na Hawa waliumbwa. Tunaweza kusema kwamba hii siku ya ijumaa ndiyo siku ya kuzaliwa (Birth Day) ya mwanadamu hapa duniani. Ikiwa watu wanapenda kusherehekea tarehe zao za kuzaliwa, basi ni bora kukumbuka pia iko siku inayojulikana ya mwanzo wa kuwepo mwanadamu hapa duniani.

Jinsi Adamu na Hawa walivyoumbwa   

Vitabu vitakatifu vina maelezo ya kina juu ya uumbaji wa mwanadamu kutoka kwa baba yetu Adamu. Kwanza, Biblia inaeeleza Adamu alivyoumba baada ya kuona kuwa siku aliyoumbwa ni siku ya sita. Sasa inaeleza jinsi alivyoumbwa.

“Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai” Mwanzo 2:7.

Qur’an Tukufu inakubaliana na maelezo ya Biblia kwamba Adamu aliumbwa kutoka katika mavumbi ya ardhi. 

وَلَقَدْ‭ ‬خَلَقْنَا‭ ‬الْإِنسَانَ‭ ‬مِن‭ ‬سُلَالَةٍ‭ ‬مِّن‭ ‬طِينٍ

 

“Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asili ya udongo” (Sura ya 23:12).

وَلَقَدْ‭ ‬خَلَقْنَا‭ ‬الْإِنسَانَ‭ ‬مِن‭ ‬صَلْصَالٍ‭ ‬مِّنْ‭ ‬حَمَإٍ‭ ‬مَّسْنُونٍ

 

“Na tulimuumba mtu kwa udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyotiwa sura” (Sura ya 15: 26).

 

وَإِذْ‭ ‬قَالَ‭ ‬رَبُّكَ‭ ‬لِلْمَلَائِكَةِ‭ ‬إِنِّي‭ ‬خَالِقٌ‭ ‬بَشَرًا‭ ‬مِّن‭ ‬صَلْصَالٍ‭ ‬مِّنْ‭ ‬حَمَإٍ‭ ‬مَّسْنُونٍ

فَإِذَا‭ ‬سَوَّيْتُهُ‭ ‬وَنَفَخْتُ‭ ‬فِيهِ‭ ‬مِن‭ ‬رُّوحِي‭ ‬فَقَعُوا‭ ‬لَهُ‭ ‬سَاجِدِينَ

 

“Na Mola wako mlezi alipowaambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyotiwa sura. Basi nitakapomkamilisha na nikampulizia roho yangu, basi mumwangukie kumsujudia.” (Sura ya 15:28-29).

Kutokana na aya hizi ndani ya Biblia na Qur’an tunagundua kwamba, Adamu aliumbwa kwa udongo (mavumbi ya ardhi) na Mwenyezi Mungu akampulizia pumzi akawa nafsi hai. Hii ni kinyume kabisa na nadharia ya wanasayansi wanaotuambia kwamba eti mwanadamu ametokana na uibukaji (evolution) yaani mabadiliko ya muda mrefu wa miaka mingi. Na kwamba mabadiliko haya yalitokana na chembechembe ndogo (single celled organism) katika maji ambayo baadye ilikua na kuwa chembechembe nyingi (multicellular). Na kwamba chembechembe hizi badaye zilikwa kiumbe, kwanza kiluilui ndani ya maji, kisha mjusi, kisha mjusi mkubwa, kisha mnyama mkubwa mwenye mkia, kisha mkia ukakatika akawa nyani, kisha sokwe mtu, na hatimaye mtu kamili. Hili ni tusi kwetu sisi wanadamu, ingawa kwa hali ya kushangaza, wengi wetu mashuleni tumekubaliana na hadaa hii ya mwovu ibilisi. Hii ni dharau kubwa kwetu sisi na Mwenyezi Mungu muumba wetu. 

Je Mwenyezi Mungu aliagiza kuwa Siku ya Ijumaa ni siku takatifu ya Ibada?

يَا‭ ‬أَيُّهَا‭ ‬الَّذِينَ‭ ‬آمَنُوا‭ ‬إِذَا‭ ‬نُودِيَ‭ ‬لِلصَّلَاةِ‭ ‬مِن‭ ‬يَوْمِ‭ ‬الْجُمُعَةِ‭ ‬فَاسْعَوْا‭ ‬إِلَىٰ‭ ‬ذِكْرِ‭ ‬اللَّهِ‭ ‬وَذَرُوا‭ ‬الْبَيْعَ‭ ‬ذَٰلِكُمْ‭ ‬خَيْرٌ‭ ‬لَّكُمْ‭ ‬إِن‭ ‬كُنتُمْ‭ ‬تَعْلَمُونَ‭ ‬فَإِذَا‭ ‬قُضِيَتِ‭ ‬الصَّلَاةُ‭ ‬فَانتَشِرُوا‭ ‬فِي‭ ‬الْأَرْضِ‭ ‬وَابْتَغُوا‭ ‬مِن‭ ‬فَضْلِ‭ ‬اللَّهِ‭ ‬وَاذْكُرُوا‭ ‬اللَّهَ‭ ‬كَثِيرًا‭ ‬لَّعَلَّكُمْ‭ ‬تُفْلِحُونَ

“Enyi mlioamini! Kukiadhiniwa kwa ajili ya Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kumtaja Mwenyezi Mungu na acheni biashara. Kufanya hivi ni bora kwenu. Ikiwa mnajua (hivi basi fanyeni). Na itakapokwisha Sala, tawanyikeni katika ardhi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi, (ili msipate kufanya mabaya), ili mpate kufaulu.” (Qur’an 62:9-10)

Hii ndiyo aya moja tu ndani ya Qur’an inayotaja siku ya Ijumaa. Hakuna aya nyingine inayotaja ijumaa kwa namna yo yote ile, au kuinasibisha na maswala ya ibada. Uchunguzi wa haraka haraka wa aya unaonyesha kwamba. Wakati aya inashuka, tayari ibada ya kukusanyika katika siku ya ijumaa ilikuwa ikifanyika. Tafsiri ya aya hii inaelezwa na Shekhe Maududi Sayyid Abul Ala Maududi Katika Tafsir yake, Tafhim Al-Qur’an kwamba;

“Kuna mambo matatu ya kuzingatia katika sentensi hii,

Kwamba inahusisha adhana (wito) kwa ibada.

Kwamba ibada hiyo inatakiwa kufanyika siku ya Ijumaa na

Kwamba mambo haya hayakutajwa ili kupendekeza kwamba adhana yapaswa kutolewa ili kuja katika ibada na ibada hiyo yapaswa kufanyika siku ya Ijumaa, lakini mtindo wa uandishi na muktadha wa aya hii unaonyesha kwamba, adhana kwa ajili ya ibada na ibada yenyewe ya ijumaa tayari vilikuwa vikifanyika. Hata hivyo inaonyesha kwamba ni watu ndiyo ambao walikuwa hawajali ibada hiyo kwa maana kwamba, walipokuwa wakisikia adhana walikuwa hawaharakishi kwenda ibadani, badala yake walisalia wakiendelea na shughuli zao za kidunia na biashara. Hivyo Mwenyezi Mungu aliteremsha aya hizi ili kuwafanya waone umuhimu na kuthamini adhana  na ibada na waharakishe kutekeleza ibada kama wajibu….(adhana hii kwa ajili ya ibada haina tofauti na adhana inayotolewa mara tano kila siku katika msikiti, lakini hakuna mahala ndani ya Qur’an Allah aliamrisha ni maneno gani yatolewe ndani ya adhana hiyo, wala Allah hajafundisha namna gani adhana itolewe)” (Maududi Sayyid Abul Ala Maududi, Tafhim Al-Qur’an, Tafsir juu ya Qur’an Sura ya 62:9-10)

Wanachuoni wote wa Kiislam wanakubaliana kwamba, hakuna mahala ndani ya Qur’an ambapo Allah (s.w) ameamrisha watu kufanya ibada maalumu katika siku ya ijuma, au kuitenga siku ya Ijumaa kuwa takatifu (yaani kwa ajili ya ibada ya Mwenyezi Mungu tu). Shekhe Maududi anasema kwamba, aya hii haikutolewa ili kuamrisha ibada katika siku ya Ijumaa isipokuwa ibada hiyo ya ijumaa ilikuwepo toka zamani hata kabla ya kushuka kwa aya hii. Na kwamba adhana inayotajwa hapa haina tofauti na adhana zingine zote za kila siku. Ikiwa Allah hajaamrisha kuwa siku ya Ijumaa itengwe kama siku takatifu ya ibada, basi itakuwa ni jambo la muhimu kuangalia kwamba jambo hili la kuifanya siku ya Ijumaa kuwa siku maalumu ya ibada lilitoka wapi ndani ya Uislam? Hebu tuichunguze historia ya Uislamu.

Dini ya Uislamu ilianzisha na mtume Muhammad (s.a.w) mnamo mwaka wa 610 BK. Wakati ambapo Muhammad alijitenga kwa ajili ya kufanya ibada ya faragha katika pango la mlima Hira huko Makka. Katika Mwezi wa Ramadhani mnamo tarehe 17 siku ya jumatatu ya mwaka huo (Tazama Tarekhe Al –Rusul wa-l-Muluk, Abu Ja’far Muhammad bin Jarir Al-Tabari’, uk 1143 na Qurqn 8:41). 

Muhammad akiwa pangoni alitokewa na mtu ambaye hakujua ametokea wapi. Akambana na kumwambia soma, Muhammad akasema, mimi sijui kusoma kwani si miongoni mwa wenye kusoma, akarudia mara ya pili akamwambia tena soma, Muhammad akarudisha jawabu lilelile. Ndipo mtu huyo alipombana mara ya tatu na kumwambia “Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba…” (Maisha ya Mtume Muhammad, Shekhe Abdallah Sareh Farsy, uk 5).

Baada ya miaka mitatu Muhammad alianza kutangaza dini ya Uislamu na wa kwanza kuingia katika Uislamu akawa mkewe bibi Khadija. Muhammad aliendelea kutangaza dini kwa wakazi wa mji wa Makka bila mafanikio kwa muda wa miaka 12 akifanikiwa kupata wafuasi wachache tu. Kwa muda huu wote wa miaka 12 hakukuwa na ibada ya siku ya ijumaa mpaka alipohamia katika mji wa Madina katika mwaka wa 612. Akiwa Madina ndipo kwa mara ya kwanza Waislamu walianza kusimamisha sala ya ijumaa kama anavyoeleza mwana historia, At Twabari’ katika Tarekhe Twabariy.

ذكر‭ ‬ما‭ ‬كان‭ ‬من‭ ‬الأمور‭ ‬المذكورة‭ ‬في‭ ‬أول‭ ‬سنة‭ ‬من‭ ‬الهجرة

قال‭ ‬أبو‭ ‬جعفر‭: ‬قد‭ ‬مضى‭ ‬ذكرنا‭ ‬وقت‭ ‬مقدم‭ ‬النبي‭ ‬ص‭ ‬المدينة،‭ ‬وموضعه‭ ‬الذي‭ ‬نزل‭ ‬فيه‭ ‬حين‭ ‬قدمها،‭ ‬وعلى‭ ‬من‭ ‬كان‭ ‬نزوله،‭ ‬وقدر‭ ‬مكثه‭ ‬في‭ ‬الموضع‭ ‬الذي‭ ‬نزله،‭ ‬وخبر‭ ‬ارتحاله‭ ‬عنه،‭ ‬ونذكر‭ ‬الآن‭ ‬ما‭ ‬لم‭ ‬نذكر‭ ‬قبل‭ ‬مما‭ ‬كان‭ ‬من‭ ‬الأمور‭ ‬المذكورة‭ ‬في‭ ‬بقية‭ ‬سنة‭ ‬قدومه،‭ ‬وهي‭ ‬السنه‭ ‬الاولى‭ ‬من‭ ‬الهجره‭.‬

فمن‭ ‬ذلك‭ ‬تجميعه‭ ‬ص‭ ‬بأصحابه‭ ‬الجمعة،‭ ‬في‭ ‬اليوم‭ ‬الذي‭ ‬ارتحل‭ ‬فيه‭ ‬من‭ ‬قباء،‭ ‬وذلك‭ ‬أن‭ ‬ارتحاله‭ ‬عنها‭ ‬كان‭ ‬يوم‭ ‬الجمعة‭ ‬عامدا‭ ‬المدينة،‭ ‬فأدركته‭ ‬الصلاة،‭ ‬صلاة‭ ‬الجمعة‭ ‬في‭ ‬بني‭ ‬سالم‭ ‬بن‭ ‬عوف،‭ ‬ببطن‭ ‬واد‭ ‬لهم‭- ‬قد‭ ‬اتخذ‭ ‬اليوم‭ ‬في‭ ‬ذلك‭ ‬الموضع‭ ‬مسجدا‭- ‬فيما‭ ‬بلغني‭- ‬وكانت‭ ‬هذه‭ ‬الجمعة،‭ ‬أول‭ ‬جمعة‭ ‬جمعها‭ ‬رسول‭ ‬الله‭ ‬صَلَّى‭ ‬اللَّهُ‭ ‬عَلَيْهِ‭ ‬وَسَلَّمَ‭ ‬في‭ ‬الإسلام،‭ ‬

“Tumekwisha kutaja tarehe ambayo mtume aliwasili Madina, mahali alipokaa wakati alipowasili, watu aliokaa nao, muda wa kukaa kwake sehemu hiyo na kuondoka kwake hapo. Sasa tutataja matukio mengine muhimu ya mwaka huo, mwaka wa kwanza wa Hijira. Miongoni mwa haya ni kufanya ibada katika siku ya Ijumaa pamoja na masahaba zake katika siku aliyotoka Quba kwenda Madina. Siku hiyo ilikuwa siku ya Ijumaa, na muda wa sala ukawadia—sala ya Ijumaa—ukamfikia akiwa katika mtaa wa Banu Salim bin Auf. Hii ndiyo ilikuwa sala ya Ijumaa ya kwanza kusaliwa katika Uislam (Tarekhe Al –Rusul wa-l-Muluk, Abu Ja’far Muhammad bin Jarir Al-Tabari’, uk 1019).

Hivyo, kwa mujibu wa historia tunaona kwamba ibada katika siku ya ijumaa imeanza kufanyika miaka 12 baada ya dini ya uislamu kutangazwa, na kwamba ibada ya kwanza ya ijumaa imefanywa katika mji wa Madina baada ya mtume kuhamia huko. Hoja ya msingi itakuwa kuchunguza ni nani hasa alianzisha ibada hii? Na je, ibada katika siku hiyo ya ijumaa ilikuwa amrisho la Mwenyezi Mungu au watu tu walikaa na kujitungia? Turejee tena katika vitabu vya historia ya Uislamu. Tunaambiwa katika Tasfri ya Qur’an ya Maududi kwamba ibada katika siku ya ijumaa ilikuwepo ikifanywa na wapagani wa mji wa Madina kabla ya Uislamu kuja. Shekhe Maududi anasema kwamba;

“Ijumaa ni neno la Kiislamu. Wakati wa zama za Jahiliya Waarabu waliita siku hii kuwa siku ya Arubah. Katika Uislam zama ilipofanywa kuwa siku ya kujumuika kwa Waislam ilibadilishwa jina na kuitwa siku ya Ijumaa. Ingawa kulingana na wana historia Kab bin Luayy, au Qusayy bin Kilab, pia walitumia jina hili (Ijumaa) kwa siku hii. Kwa sababu alikuwa akiwakusanya Makuraishi katika siku hii (ya Arubah). Hivyo kwa tendo hili jina la kale la siku halikubadilika, na Waarabu waliendelea kuiita siku ya Arubah. Badiliko halisi lilitokea pale Waislam walipoibadilisha jina na kuiita Ijumaa. (Maududi Sayyid Abul Ala Maududi, Tafhim Al-Qur’an, Tafsir juu ya Qur’an Sura ya 62:9-10).

Hivyo tunaona kwamba jina ijumaa halikwa jina asili la lugha ya Kiarabu isipokuwa ni jina ambalo lilipatikana baadaye wakati Uislamu ulipokuja. Siku hii ya ijumaa zamani wakati wa Jahiliya ilikuwa ikiitwa siku ya Arubah. Kulingana na mwanachuoni Imam ibn Hajar al-Asqalani siku za juma kabla ya Uislam kwa Kiarabu zilijulikana kama ifuatavyo;

أسماء‭ ‬الأيام‭ ‬السبعة‭ ‬بعد‭ ‬أن‭ ‬كانت‭ ‬تسمى‏‭:‬

‭ ‬أول،‭ ‬أهون،‭ ‬جبار،‭ ‬دبار،‭ ‬مؤنس،‭ ‬عروبة،‭ ‬شبار

Jumapili (Yaum Awwal), Jumatatu (Yaum Ahwan), Jumanne (Yaum Jubar), Jumatano (Yaum Dubar), Al-Khamis (Yaum Mu’nis), Ijumaa (Yaum Arubah), Juma mosi (Yaum Shibar)

Kisha Imam ibn Hajar al-Asqalani, akinukuu hadithi ya Abd bin hamiid, anaendelea kusema;

‏ويليه‭ ‬ما‭ ‬أخرجه‭ ‬عبد‭ ‬بن‭ ‬حميد‭ ‬عن‭ ‬ابن‭ ‬سيرين‭ ‬بسند‭ ‬صحيح‭ ‬إليه‭ ‬في‭ ‬قصة‭ ‬تجميع‭ ‬الأنصار‭ ‬مع‭ ‬أسعد‭ ‬بن‭ ‬زرارة،‭ ‬وكانوا‭ ‬يسمون‭ ‬يوم‭ ‬الجمعة‭ ‬يوم‭ ‬العروبة،‭ ‬فصلى‭ ‬بهم‭ ‬وذكرهم‭ ‬فسموه‭ ‬الجمعة‭ ‬حين‭ ‬اجتمعوا‭ ‬إليه،‭ ‬ذكره‭ ‬ابن‭ ‬أبي‭ ‬حاتم‭ ‬موقوفا‏‭.... ‬لأن‭ ‬كعب‭ ‬بن‭ ‬لؤي‭ ‬كان‭ ‬يجمع‭ ‬قومه‭ ‬فيه‭ ‬فيذكرهم‭ ‬ويأمرهم‭ ‬بتعظيم‭ ‬الحرم‭ ‬ويخبرهم‭ ‬بأنه‭ ‬سيبعث‭ ‬منه‭ ‬نبي‭... ‬إن‭ ‬قصيا‭ ‬هو‭ ‬الذي‭ ‬كان‭ ‬يجمعهم‭ ‬ذكره‭ ‬ثعلب‭ ‬في‭ ‬أماليه‏‭. ‬‏وقيل‭ ‬سمي‭ ‬بذلك‭ ‬لاجتماع‭ ‬الناس‭ ‬للصلاة‭ ‬فيه،‭ ‬وبهذا‭ ‬جزم‭ ‬ابن‭ ‬حزم‭ ‬فقال‏‭: ‬إنه‭ ‬اسم‭ ‬إسلامي‭ ‬لم‭ ‬يكن‭ ‬في‭ ‬الجاهلية‭ ‬وإنما‭ ‬كان‭ ‬يسمى‭ ‬العروبة‭...‬

“ Ansar (Watu wa Madina) Walikuwa wakikusanyika pamoja na As’wad bin Zurarah  na wakiita siku ya Aruba kuwa Jumaa’ (kusanyiko) na wakasali kwake na hivyo wakawa wanaiita siku ya Ijumaa (kusanyiko) kisha wakaendelea kukusanyika kwake…hii ni kwa sababu,  Kab bin Luway alikuwa akiwakusanya watu wake (Makuraish) katika siku hiyo na akiwaamrisha kuiadhimisha na kuifanya kuwa takatifu na akwaambia kwamba karibuni atatumwa kwao nabii…hakika jina la Kiislam (Ijumaa) halikuwepo wakati wa Jahiliya na kwa hakika ilikuwa ikiitwa Arubah…Tha’lab anasema kwamba Jumua’ iliitwa hivyo kwa sababu Makuraish walikuwa wakikusanyika pamoja kwa Qusay katika Dar an-Nadwa”  (Fat’h al-Bari, Ibn Hajar al-Asqalani, Mlango wa Ijumaa).

Huyu Kab bin Lu’ay ni babu wa saba wa Muhammad (al Jadu saabiu’). Hii inaleta maana kwamba walikuwa wakikusanyika katika siku ya Arubah (ambayo baadaye ilibadilishwa jina na kuitwa Ijumaa na Waislam) miaka mingi sana kabla ya Uislam kuja. Sasa tuangalie ni kwa nini hasa Waislam katika mji wa Madina walichagua kufanya ibada zao katika siku ya Arubah mapema kabisa hata kabla ya mtume kuhamia huko?

Mwanzo wa ibada katika siku ya Ijumaa katika mji wa Madina

Hitoria inatuambia kwamba, Muhammad aliendelea kupata upinzani katika kueneza dini ya Uislam katika mji wa Makka. Siku moja wakati wa Hija akiwa Aqabah huko Mina, alikutana na kundi la watu kutoka kabila la Al-Khazraj wakazi wa mji wa Madina. Muhammad aliwahubiria watu hawa na kuwasomea Qur’an. Watu hawa waliamini mafundisho ya Muhammad na kumwamini kama mtume kisha wakasema na kumwambia mtume;

“Tumewaacha watu wetu wakiwa maadui wao kwa wao, hakuna watu walio na uadui na chuki baina yao kama watu wetu (watu wa Madina). Tunatarajia Allah atawaunganisha kupitia wewe, hivyo tutakwenda kuwaambia, na kuwaita wakufuate wewe, na kuwaomba wafuate kile tulichokikubali kutoka kwako kulingana na dini uliyoileta. Ikiwa Allah atawaunganisha watu hawa kupitia uongozi wako, hakutakuwa na mtu atakayekuwa na nguvu kukushinda wewe” (Qiswas al-Anbiyau, Ibn Hisham).

Watu hawa ambao inakubaliwa katika historia ya Uislam ndiyo walikuwa Ansar (watetezi wa mtume) wa kwanza katika watu wa Madina kutoka ukoo wa banu Al-Khazraj ni “As’ad bin Zurarah, bin Uday, Auf bin Al-Harith bin Rafa’h,  Rafi bin Malik bin Al-Ajlan, Qutbah bin Amir bin Haeedah, Uqbah bin Amir bin Naaby na Jabir bin Abdullah bin Ri’ab (Qiswas A-Anbiyau, Ibin Hisham).

Ibn Hisham anaeleza kwamba watu hawa waliporudi nyumbani kwao Madina walianza kuhubiri kwa watu wa nyumbani kwao kila mtu katika jamaa zake wa karibu mpaka ikafikia kwamba, “ikajulikana miongoni mwao kwamba hakukuwa na nyumba kati ya ndugu zao isipokuwa wote walisilimu na kwamba mtume ametajwa katika nyumba hiyo” (Ibn Hisham).

Baadaye alitumwa sahaba wa mtume akijulikana kwa jina la Mus’ab bin Umayr kama balozi wa Uislam katika mji wa Madina  ili kuuanda mji huo kwa Hijra ya Mtume. Bwana Mus’ab alipokelewa vizuri na bwana As’ad bin Zurara na kwa pamoja walianza kueneza Uislam kwa nguvu katika mji wa Madina. Wakazi wengi wa Madina walisilimu ikiwa ni pamoja na watu mashuhuri kama Sa’d bin Mu’adh, Usayd bin Hudayr na Sa’d bin Ubadah. Watu hawa Waislam walipozidi kuwa wengi huko Madina ndiyo kwa mara ya kwanza wakafanya kikao ili kujitafutia siku maalumu ya kufanya ibada. Maamuzi ya kikao hicho yamesimuliwa na wanachuoni wa historia ya Kiislam mbali mbali, na hapa nitawanukuu wachache.

Azzamakshari katika Al-Kashaf yake ananukuu hadithi ya Muhammad bin Siribn kusema;

‏قوله‏‭: (‬‏فهدانا‭ ‬الله‭ ‬له‏‭)‬‏‭ ‬يحتمل‭ ‬أن‭ ‬يراد‭ ‬بأن‭ ‬نص‭ ‬لنا‭ ‬عليه،‭ ‬وأن‭ ‬يراد‭ ‬الهداية‭ ‬إليه‭ ‬بالاجتهاد،‭ ‬ويشهد‭ ‬للثاني‭ ‬ما‭ ‬رواه‭ ‬عبد‭ ‬الرزاق‭ ‬بإسناد‭ ‬صحيح‭ ‬عن‭ ‬محمد‭ ‬بن‭ ‬سيربن‭ ‬قال‭ ‬‏”‏‭ ‬جمع‭ ‬أهل‭ ‬المدينة‭ ‬قبل‭ ‬أن‭ ‬يقدمها‭ ‬رسول‭ ‬الله‭ ‬صلى‭ ‬الله‭ ‬عليه‭ ‬وسلم‭ ‬وقبل‭ ‬أن‭ ‬تنزل‭ ‬الجمعة،‭ ‬فقالت‭ ‬الأنصار‏‭:  ‬إن‭ ‬لليهود‭ ‬يوما‭ ‬يجتمعون‭ ‬فيه‭ ‬كل‭ ‬سبعة‭ ‬أيام،‭ ‬وللنصارى‭ ‬كذلك،‭ ‬فهلم‭ ‬فلنجعل‭ ‬يوما‭ ‬نجتمع‭ ‬فيه‭ ‬فنذكر‭ ‬الله‭ ‬تعالى‭ ‬ونصلي‭ ‬ونشكره‏‭. ‬فجعلوه‭ ‬يوم‭ ‬العروبة،‭ ‬واجتمعوا‭ ‬إلى‭ ‬أسعد‭ ‬بن‭ ‬زرارة‭ ‬فصلى‭ ‬بهم‭ ‬يومئذ،‭ ‬وأنزل‭ ‬الله‭ ‬تعالى‭ ‬بعد‭ ‬ذلك‭ ‬‏‭(‬‏إذا‭ ‬نودي‭ ‬للصلاة‭ ‬من‭ ‬يوم‭ ‬الجمعة‏‭)‬‏‭ ‬الآية

Walikusanyika watu wa Madina kabla mtume (s.a.w) hajatelemshiwa siku ya ijumaa wakasema Maansar; ‘Wayahudi wanakusanyika kila siku ya Sabato, na Manasara pia wanayo siku yao ya ibada (siku ya juma pili). Haya natujifanyie na sisi siku ambayo tutakusanyika na kumtaja Mwenyezi Mungu na kusali na kumshukuru. Wakaijalia siku ya Arubah (kuwa siku yao ya ibada). Wakakusanyika siku hiyo katika nyumba ya As’ad bin Zurarah. Kisha baada ya hapo Allah akatelemsha “Kukiadhiniwa kwa ajili ya Sala siku ya Ijumaa, …” (sura ya 62:9) (Tafsir Azzamakshar juu ya Sura ya 62:9-10).

Baada ya miaka mingi kupita na bwana As’ad bin Zurarah kuwa alikwisha kufa, Ka’b bin Maliki aliyekuwepo katika tukio hili la kuanzishwa kwa ibada ya Ijumaa katika Uislam aliendelea kukumbuka tukio hili. Hadithi ya Ka’b bin Maliki inasema;

حَدَّثَنَا‭ ‬قُتَيْبَةُ‭ ‬بْنُ‭ ‬سَعِيدٍ،‭ ‬حَدَّثَنَا‭ ‬ابْنُ‭ ‬إِدْرِيسَ،‭ ‬عَنْ‭ ‬مُحَمَّدِ‭ ‬بْنِ‭ ‬إِسْحَاقَ،‭ ‬عَنْ‭ ‬مُحَمَّدِ‭ ‬بْنِ‭ ‬أَبِي‭ ‬أُمَامَةَ‭ ‬بْنِ‭ ‬سَهْلٍ،‭ ‬عَنْ‭ ‬أَبِيهِ،‭ ‬عَنْ‭ ‬عَبْدِ‭ ‬الرَّحْمَنِ‭ ‬بْنِ‭ ‬كَعْبِ‭ ‬بْنِ‭ ‬مَالِكٍ،‭ - ‬وَكَانَ‭ ‬قَائِدَ‭ ‬أَبِيهِ‭ ‬بَعْدَ‭ ‬مَا‭ ‬ذَهَبَ‭ ‬بَصَرُهُ‭ ‬عَنْ‭ ‬أَبِيهِ،‭ ‬كَعْبِ‭ ‬بْنِ‭ ‬مَالِكٍ‭ ‬أَنَّهُ‭ ‬كَانَ‭ ‬إِذَا‭ ‬سَمِعَ‭ ‬النِّدَاءَ،‭ ‬يَوْمَ‭ ‬الْجُمُعَةِ‭ ‬تَرَحَّمَ‭ ‬لأَسْعَدَ‭ ‬بْنِ‭ ‬زُرَارَةَ‭ ‬‏‭.‬‏‭ ‬فَقُلْتُ‭ ‬لَهُ‭ ‬إِذَا‭ ‬سَمِعْتَ‭ ‬النِّدَاءَ،‭ ‬تَرَحَّمْتَ‭ ‬لأَسْعَدَ‭ ‬بْنِ‭ ‬زُرَارَةَ‭ ‬قَالَ‭ ‬لأَنَّهُ‭ ‬أَوَّلُ‭ ‬مَنْ‭ ‬جَمَّعَ‭ ‬بِنَا‭ ‬فِي‭ ‬هَزْمِ‭ ‬النَّبِيتِ‭ ‬مِنْ‭ ‬حَرَّةِ‭ ‬بَنِي‭ ‬بَيَاضَةَ‭ ‬فِي‭ ‬نَقِيعٍ‭ ‬يُقَالُ‭ ‬لَهُ‭ ‬نَقِيعُ‭ ‬الْخَضِمَاتِ‭ ‬‏‭.‬‏‭ ‬قُلْتُ‭ ‬كَمْ‭ ‬أَنْتُمْ‭ ‬يَوْمَئِذٍ‭ ‬قَالَ‭ ‬أَرْبَعُونَ‭ ‬‏‭.‬

“Imesimuliwa na AbdurRahman bin Ka’ab bin Maliki kutoka kwa baba yake: amesema; wakati Ka’b bin Maliki aliposikia wito kwa ajili ya sala (adhana) katika siku ya Ijumaa, akamwombea As’ad bin Zurarah. Nikamwuliza, kwanini unaposikia adhana humsalia As’ad bin Zurarah? Akanijibu, hii ni kwa sababu yeye ndiye aliyetusalisha sala ya Ijumaa kwa mara ya kwanza….Nikamuuliza, je mlikuwa wangapi siku hiyo? Akajibu, tulikuwa arobaini” (Sunan Abu Dawud, Hadithi Namba 1069).

Hivyo, ni wazi kabisa kulingana na historia, siku hii ya Ijumaa siyo amrisho la Mwenyezi Mungu la kufanya ibada, isipokuwa imeteuliwa kutokana na matamanio ya watu, Waislam wa mwanzo katika mji wa Madina. Na hoja yao kubwa ikiwa ni kujitofautisha na Wayahudi na Wakristo. Tatizo moja walilokuwa nalo watu hawa ni kwamba, hawakujua kuwa Mwenyezi Mungu katika Vitabu vitakatifu kabla ya Uislamu alikuwa ameaagiza watu wake kukusanyika katika siku ya Sabato kama kumbukumbu ya uumbaji wake na kama siku iliyobarikiwa na siku takatifu ya ibada kama tulivyoona huko juu. Maududi katika Tafsri yake, Tafhiim al-Qur’an anasema kwamba;

“Kabla ya Uislam kuweka kando siku moja ya juma kama siku ya ibada na kuichukulia kama ishara ya jamii ya waumini lilikuwa jambo lililopendelewa miongoni mwa watu wa kitabu (Wayahudi na Wakristo) kuwa na siku ya ibada iliyowatambulisha. Miongoni mwa Wayahudi Sabato (jumamosi) ilisimikwa kwa ajili ya kusudi hili, kwa sababu katika siku hii, Mwenyezi Mungu aliwaokoa wana wa Israeli kutoka utumwani mwa Farao. Ili kujitofautisha na Wayahudi, Wakristo walichagua siku ya Jumapili kama nembo ya utambuisho wao. Ingawa (siku hii ya jumapili) haikupendekezwa na manabii wala Yesu mwenyewe, wala haikutajwa mahali popote katika Injili, ingawa Wakristo wanaamini kwamba baada ya kifo chake katika msalaba, Yesu alifufuka kutoka kaburini siku hii na kupaa mbinguni. Kwa uelewa huu Wakristo baadaye waliifanya kuwa siku ya ibada, na kisha katika mwaka 321 B.K. mtawala wa Kirumi aliifanya kuwa siku kuu kwa amri. Ili kujitofautisha na jamii hizi mbili Waislam walichagua siku ya Ijumaa kama siku ya ibada kinyume na Jumamosi na Jumapili” (Maududi, Tafhiim al-Qur’an,  juu ya Sura ya 62:9-10).

Mambo ya kuzingatia katika maelezo ya Shekhe Maududi ni kwamba;

Kulingana na Maandiko matakatifu, Mwenyezi Mungu aliwaagiza wana wa Israelikupumzika na kufanya ibada katika siku ya sabato. Ingawa sababu pekee ya kutolewa kwa pumziko la siku ya Sabato Maududi anaeleza kuwa ni kwa sababu walikuwa watumwa katika nchi ya Misri (Torati 5:12--15), lakini ukweli ni kwamba hii haikuwa sababu pekee. Sababu nyingine ya Mwenyezi Mungu kufanya siku ya Sabato kama siku ya pumziko la ibada ni kama tulivyoona huko juu kwamba; Mwenyezi Mungu alitaka watu wakumbuke kuwa mbingu na dunia na vyote vilivyomo ni kazi ya mikono yake Mungu (Kutoka 8:11) na wala siyo kazi ya uibukaji (evolution) na kwamba, ni Ishara kati ya Mungu na watu wake (Ezekieli 20:20).

Maududi anaeleza wazi wamba, Wakristo wanaoabudu katika siku ya jumapili walijichagulia wenyewe kufanya hivyo ili kujitofautisha na Wayahudi, siyo agizo la Mwenyezi Mungu, Manabii wala Yesu mwenyewe hakuagiza hivyo. Kisha anasema, ibada ya siku ya Jumapili ilitiwa nguvu kwa amri ya mfalme wa Kirumi aliyekuwa akiitwa Kostantino.

Maududi anakubaliana na wanachuoni wengine wa Kiislamu kwamba, siku ya Ijumaa pia ni maamuzi ya watu (Waislamu wa Madina), kwa sababu ya kutaka kujitofautisha na Wayahudi na Wakristo. Wanachuoni pia wameeleza kwamba, siku hiyo ya Ijumaa zamani ilikuwa inaitwa Arubah ambayo iliadhimishwa na wapagani wa Kikuraishi katika mji wa Makka wakiongozwa na Kab bin Lu’ayy zamani kabisa kabla ya Uislamu kuja. Hivyo kwa mujibu wahistoria na wanachuoni wa Kiislamu, Jumapili na Ijumaa zote ni siku za kipagani ambazo zimeingizwa tu katika dini za Kikristo na Uislamu.

Je adhana katika Uislam ilitoka wapi?

Tumeona kuwa wakati Qur’an sura ya 62:9 iliposhuka, tayari kulikuwa na adhana, na kwamba aya haikushuka ili kuamrisha adhana. Turudie kuisoma tena aya hii kwa mara nyingine ili kujikumbusha;

يَا‭ ‬أَيُّهَا‭ ‬الَّذِينَ‭ ‬آمَنُوا‭ ‬إِذَا‭ ‬نُودِيَ‭ ‬لِلصَّلَاةِ‭ ‬مِن‭ ‬يَوْمِ‭ ‬الْجُمُعَةِ‭ ‬فَاسْعَوْا‭ ‬إِلَىٰ‭ ‬ذِكْرِ‭ ‬اللَّهِ‭ ‬وَذَرُوا‭ ‬الْبَيْعَ‭ ‬ذَٰلِكُمْ‭ ‬خَيْرٌ‭ ‬لَّكُمْ‭ ‬إِن‭ ‬كُنتُمْ‭ ‬تَعْلَمُونَ‭ ‬فَإِذَا‭ ‬قُضِيَتِ‭ ‬الصَّلَاةُ‭ ‬فَانتَشِرُوا‭ ‬فِي‭ ‬الْأَرْضِ‭ ‬وَابْتَغُوا‭ ‬مِن‭ ‬فَضْلِ‭ ‬اللَّهِ‭ ‬وَاذْكُرُوا‭ ‬اللَّهَ‭ ‬كَثِيرًا‭ ‬لَّعَلَّكُمْ‭ ‬تُفْلِحُونَ

“Enyi mlioamini! Kukiadhiniwa kwa ajili ya sala siku ya ijumaa, nendeni upesi kumtaja Mwenyezi Mungu na acheni biashara. Kufanya hivi ni bora kwenu. Ikiwa mnajua (hivi basi fanyeni). Na itakapokwisha sala, tawanyikeni katika ardhi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi, (ili msipate kufanya mabaya), ili mpate kufaulu.” (Qur’an 62:9-10).

Tumekwisha kuona wafasili wa aya hii wakisema kuwa wakati inashuka, tayari kulikuwa na utaratibu wa kuwaita watu kuja katika ibada kwa kuadhini. Je, utaratibu wa kuadhini ulianzaje? Twavigeukia tena vitabu vya historia ili kubaini chanzo cha adhana. Tunasoma katika Sahihi Bukhari kwamba;

حَدَّثَنَا‭  ‬مَحْمُودُ‭ ‬بْنُ‭ ‬غَيْلاَنَ،‭ ‬قَالَ‭ ‬حَدَّثَنَا‭ ‬عَبْدُ‭ ‬الرَّزَّاقِ،‭ ‬قَالَ‭  ‬أَخْبَرَنَا‭ ‬ابْنُ‭ ‬جُرَيْجٍ،‭ ‬قَالَ‭ ‬أَخْبَرَنِي‭ ‬نَافِعٌ،‭ ‬أَنَّ‭ ‬ابْنَ‭  ‬عُمَرَ،‭ ‬كَانَ‭ ‬يَقُولُ‭ ‬كَانَ‭ ‬الْمُسْلِمُونَ‭ ‬حِينَ‭ ‬قَدِمُوا‭ ‬الْمَدِينَةَ‭  ‬يَجْتَمِعُونَ‭ ‬فَيَتَحَيَّنُونَ‭ ‬الصَّلاَةَ،‭ ‬لَيْسَ‭ ‬يُنَادَى‭ ‬لَهَا،‭  ‬فَتَكَلَّمُوا‭ ‬يَوْمًا‭ ‬فِي‭ ‬ذَلِكَ،‭ ‬فَقَالَ‭ ‬بَعْضُهُمْ‭ ‬اتَّخِذُوا‭  ‬نَاقُوسًا‭ ‬مِثْلَ‭ ‬نَاقُوسِ‭ ‬النَّصَارَى‏‭.‬‏‭ ‬وَقَالَ‭ ‬بَعْضُهُمْ‭ ‬بَلْ‭ ‬بُوقًا‭  ‬مِثْلَ‭ ‬قَرْنِ‭ ‬الْيَهُودِ‏‭.‬‏‭ ‬فَقَالَ‭ ‬عُمَرُ‭ ‬أَوَلاَ‭ ‬تَبْعَثُونَ‭ ‬رَجُلاً‭  ‬يُنَادِي‭ ‬بِالصَّلاَةِ‏‭.‬‏‭ ‬فَقَالَ‭ ‬رَسُولُ‭ ‬اللَّهِ‭ ‬صلى‭ ‬الله‭ ‬عليه‭ ‬وسلم‭ ‬‏”‏‭ ‬يَا‭ ‬بِلاَلُ‭ ‬قُمْ‭ ‬فَنَادِ‭ ‬بِالصَّلاَةِ‭ ‬‏”

“Imesimuliwa na ibn Umar: Waislamu walipofika Madina, walikuwa wakikusanyika kwa ajili ya sala na wakikadiria muda wa kukusanyika. Wakati huo kuadhini kwa ajili ya sala kulikwa hakujaanzishwa bado. Walijadili tatizo hili kuhusiana na wito kwa ajili ya sala, baadhi ya watu wakapendekeza wawe wanapiga kengele kama walivyokuwa wakifanya Wakristo, wengine wakapendekeza kupiga baragumu kama pembe iliyokuwa ikipigwa na Wayahudi, lakini Umar alikuwa mtu wa kwanza kupendekeza kwamba, mtu mmoja angekuwa anawaaita wengine kwa ajili ya sala. Hivyo mtume wa Allah (s.a.w) akampendekeza Bilal kusimama na kutoa adhana.” (Sahihi Bukhari, Mlango wa Adhana, hadithi namba 604).

Yaonekana kwamba mtume alipendelea baragumu la Wayahudi lakini baadaye hakuridhika nalo. Kisha “akaamuru kutengenezwe kengele ambayo itakuwa ikipigwa ndipo Waislamu wakusanyike kwa ajili ya sala” (Ibn Hisham).

Ni kitu gani kilipelekea mtume amchague Bilal kutoa adhana badala ya mapendekezo yaliyotolewa ya kutumia kengele na baragumu vitu ambavyo vinatumiwa na  Wakristo na Wayahudi? Kabla ya pendekezo la mtume Abdullah bin Zayd bin Tha’laba bin Abdu Rabbihi aliota ndoto akamwambia mtume kwamba; 

“Alipita mtu mbele yangu amevalia mavazi mawili ya kijani akiwa amebeba kengele mkononi mwake na nikamwomba aniuzie. Aliponiuliza nilitaka kengele hiyo kwa ajili ya nini , nilimwambia kwamba ilikuwa kwa ajili ya kuwaita watu katika sala. Ndipo aliponionyesha njia bora ya kuwaita watu kwa ajili ya sala, kwamba ilitakiwa kusema. “Allah Akbar, Allah Akbar, Ash’hadu la Illha ila Llha, Ash’had anna Muhammad Rasulu llah. Hayya allah sala, hayya allah sala, Allah Akbar, Allah Akbar. La Ilah ila llah. Mtume alipoambiwa maneno haya akasema, ‘hiyo ndoto ni ya kweli, na kwamba kama Mwenyezi Mungu atapenda (Inshaallah), atakwenda kumwambia Bilal ili awe akitoa adhana kwa kutumia maneno hayo” (Ibn Hisham).

Haya ndiyo maneno ya adhana toka siku hiyo na ndivyo ilivyo leo katika Uislamu. Chanzo chake kama ilivyokuwa kwa siku yenyewe ya ijumaa ni mipango ya watu tu, na wala siyo maagizo ya Mwenyezi Mungu. Jambo la kujiuliza ni iwapo kweli ndoto hii ilitoka kwa Mwenyezi Mungu, au yalikuwa ni matamanio ya Abdullah bin Zayd kumdanganya mtume. Na kwa nini Mwenyezi Mungu asimfunulie mtume jambo hili mpaka amruke kwenda kumpatia ndoto hiyo Abdullah bina Zayd. Je, huyu mtu ana nafasi gani katika Uislamu? Je, yeye naye ni Nabii? Maana kama amepewa ufunuo wa adhana na Mwenyezi Mungu kwa njia ya ndoto basi ni hakika anastahili kuwa nabii. Hili haliwezi kukubalika kwa Waislamu kuwa bwana Abdullah bin Zayd naye ni nabii. Hivyo basi kulingana na uchunguzi huu wa historia ya Uislamu, ibada katika siku ya ijumaa ni matamanio ya wanadamu. Rafiki yangu kwa nini sasa usifanye uamzi wa kufuata amri ya Mwenyezi Mungu aliyetuamuru kupitia vitabu vyake vitakatifu kupumzika na kufanya ibada katika siku ya Sabato, siku ya Jumamosi? Ni heri kumtii Mwenyezi Mungu kuliko kuwatii wanadamu.

Sababu ya Kushuka kwa Sura ya 62 (Surat Jumua’) ndani ya Qur’an.

Kama tulivyoona hapo juu, sura ya 62:9-10 wakati inashuka, tayari Waislamu walikuwa wakikusanyika katika siku ya Arubah ambayo baadaye walikuja kuibadilisha jina kuwa ijumaa. Tuangalie wanachuoni wa kiislam wanasemaje hasa juu ya mazingira ya kushuka kwa aya hizi. Kumbuka kama ambavyo tumekwisha kuona kwamba, zamani kabisa kabla ya Uislamu, zama za Jahiliyya, Makuraishi na makabila mengine ya Waarabu walikuwa na siku kuu iliyokuwa ikiadhimishwa na kutukuzwa, siku ya Arubah. Siku hii ilikuwa siku kubwa kibiashara pia, ambapo kulikuwa na soko kubwa (gulio) likifanyika katika siku hii. Watu waliuza na kununua katika siku hii na kulikuwa na misafara mikubwa ya wafanya biashara wakisafiri huku na huko. Tumekwisha kuona pia kwamba Waislamu wa mwanzo waliifanya siku hii kuwa siku ya ibada na kuibadilisha jina kutoka Arubah na kuiita siku ya ijumaa (siku ya kusanyiko). Kuifanya kwao kuwa siku ya ibada hakukukomesha biashara katika siku hii kabla ya dola ya Kiislamu kuanzishwa. Hivyo, Waislamu wengi waliendelea kuitukuza kama siku kuu ya kufanya biashara. Hii ilisababisha kuathiri mahudhurio ya waumini katika ibada siku ya ijumaa. Athari hizi zinaonekana wazi kabisa hasa tunapoangalia tukio ambalo mwanachuoni wa kiislamu na mfasiri mkubwa wa Qur’an, Shekhe Maududi akiwanukuu Jabir bin Abdullah, Abudllah bin Abbas, Abu Huraira, Abu Maliki na Hasan Basri, Ibn Zaid, Qatadah na Muqatil bin Hayyan kwamba;

“Siku moja msafara wa wafanya biashara kutoka Shamu uliingia Madina wakati wa sala ya ijumaa, na watu wa Madina wakaanza kucheza ngoma (kwa kuwashangilia wafanya biashara hao) katika kutangaza ujio wao. Wakati huo mtume (s.a.w) alikuwa akitoa khutuba. Walipozisikia ngoma, waumini (waliokuwa katika sala siku hiyo pamoja na mtume), wakatoka wakikimbia kuelekea Baqi ambapo msafara ulikuwa umesimama. Ni watu 12 tu ndiyo waliosalia pamoja na mtume katika ibada…” (Maududi, Tafhiim al-Qur’an juu ya sura ya 62:9-10).

Imam Bukhari ananukuu kisa hiki kutoka hadithi ya  Jabir kwamba;

وَحَدَّثَنَا‭ ‬إِسْمَاعِيلُ‭ ‬بْنُ‭  ‬سَالِمٍ،‭ ‬أَخْبَرَنَا‭ ‬هُشَيْمٌ،‭ ‬أَخْبَرَنَا‭ ‬حُصَيْنٌ،‭ ‬عَنْ‭ ‬أَبِي‭  ‬سُفْيَانَ،‭ ‬وَسَالِمِ،‭ ‬بْنِ‭ ‬أَبِي‭ ‬الْجَعْدِ‭ ‬عَنْ‭ ‬جَابِرِ‭ ‬بْنِ‭ ‬عَبْدِ‭  ‬اللَّهِ،‭ ‬قَالَ‭ ‬بَيْنَا‭ ‬النَّبِيُّ‭ ‬صلى‭ ‬الله‭ ‬عليه‭ ‬وسلم‭ ‬قَائِمٌ‭ ‬يَوْمَ‭  ‬الْجُمُعَةِ‭ ‬إِذْ‭ ‬قَدِمَتْ‭ ‬عِيرٌ‭ ‬إِلَى‭ ‬الْمَدِينَةِ‭ ‬فَابْتَدَرَهَا‭  ‬أَصْحَابُ‭ ‬رَسُولِ‭ ‬اللَّهِ‭ ‬صلى‭ ‬الله‭ ‬عليه‭ ‬وسلم‭ ‬حَتَّى‭ ‬لَمْ‭ ‬يَبْقَ‭ ‬مَعَهُ‭  ‬إِلاَّ‭ ‬اثْنَا‭ ‬عَشَرَ‭ ‬رَجُلاً‭ ‬فِيهِمْ‭ ‬أَبُو‭ ‬بَكْرٍ‭ ‬وَعُمَرُ‭ - ‬قَالَ‭ -  ‬وَنَزَلَتْ‭ ‬هَذِهِ‭ ‬الآيَةُ‭ ‬‏‭{‬‏‭ ‬وَإِذَا‭ ‬رَأَوْا‭ ‬تِجَارَةً‭ ‬أَوْ‭ ‬لَهْوًا‭ ‬انْفَضُّوا‭ ‬إِلَيْهَا‏‭}‬‏

“Imesimuliwa na Jabir bin Abdhullah: mtume (s.a.w) alikuwa akitoa khutuba siku ya ijumaa wakati msafara mkubwa kutoka Shamu ulipofika katika mji wa Madina. Masahaba wa mtume wakakimbia kwenda huko wakabaki watu 12 tu wakiwa ni pamoja na Abu Bakr na Umar; na hapo ndipo iliposhuka aya hii “na wanapoiona biashara au pumbao wanayakimbilia hayo na wakakuacha…” [Qur’an 62:11) (Sahihi Muslim, Hadithi Namba 863).

Katika Tafsir ya Twabari juu ya sura ya 62 (surat-ul- Jumua’) tunaambiwa kwamba; katika siku hiyo ya ijumaa ambayo ilikuwa siku ya gulio katika mji wa Madina, ilikuwa watu wanaposikia adhana huendelea na biashara zao tu na kupuuzia wito was sala.

حَدَّثَنَا‭ ‬مِهْرَان‭ , ‬عَنْ‭ ‬سُفْيَان‭ , ‬عَنْ‭ ‬إِسْمَاعِيل‭ ‬السُّدِّيّ‭ , ‬عَنْ‭ ‬أَبِي‭ ‬مَالِك‭ , ‬قَالَ‭ :  ‬كَانَ‭ ‬قَوْم‭ ‬يَجْلِسُونَ‭ ‬فِي‭ ‬بَقِيع‭ ‬الزُّبَيْر‭ , ‬فَيَشْتَرُونَ‭ ‬وَيَبِيعُونَ‭ ‬إِذَا‭ ‬نُودِيَ‭ ‬لِلصَّلَاةِ‭ ‬يَوْم‭ ‬الْجُمُعَة‭ , ‬وَلَا‭ ‬يَقُومُونَ‭ , ‬فَنَزَلَتْ‭ :  { ‬إِذَا‭ ‬نُودِيَ‭ ‬لِلصَّلَاةِ‭ ‬مِنْ‭ ‬يَوْم‭ ‬الْجُمُعَة

Hadithi ya Abiy Maliki: amesema; Walikuwa watu wakikaa Al-Baqi (eneo la Makaburi ya masahaba) wakiuza na kununua wakati kunapotolewa wito (adhana) kwa ajili ya sala siku ya ijumaa wala hawasimami, ndipo ikashuka aya “Enyi mlioamini! Kukiadhiniwa kwa ajili ya Sala siku ya ijumaa, nendeni upesi kumtaja Mwenyezi Mungu na acheni biashara”. (Tafsir Twabari, juu ya Sura ya 62:9-10).

Huu ndiyo muktadha hasa wa kushuka kwa aya hizi. Hivyo, tunaona kwamba sura ya 62 (Suratul Jumua’) haikushuka kwa ajili ya kuitakasa siku ya ijumaa kuwa takatifu, lakini ni kwa ajili ya kuwasisitiza waumini ili kuzingatia ibada kuliko kuacha kuabudu na kufanya biashara tu. Kumbuka kwamba ni hali halisi ya mazingira ya gulio siku hiyo ndiyo yaliwafanya watu wengi kutokuja kwa ibada. Ina maana kwamba kama kusingekuwa na soko (gulio) katka mji wa Madina katika siku ya ijuma, huenda kusingekuwa na aya hii ndani ya Qur’an. Hii ni kwa sababu, Mwenyezi Mungu hakuwa amepanga kubadilisha siku ya ibada kutoka siku aliyoibariki na kuitakasa, siku ya jumamosi (siku ya Sabato) ili aweke siku ya ijumaa. 

Mapema kabisa kabla ya Muhammad na Uislamu kuwepo, Mwenyezi Mungu alikuwa amesema.;

“Mimi sitalihalifu agano langu, Sitalibadili neno lililotoka midomoni mwangu” Zaburi 89:34.

Ni agano gani hilo ambalo alisema kuwa hatalihalifu wala kulibadili?

“Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu; nitawaleta hao nao katika mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu yangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote” (Isaya 56:6-7)

Ni wazi kwamba Mwenyezi Mungu alikusudia kuifanya siku ya Sabato kuwa agano lake siyo kwa Wayahudi tu, lakini pia kwa wageni (watu wa mataifa mengine), na kwamba agano hilo Mwenyezi Mungu alilolisema katika Zaburi 89:34 kama tulivyoona, hakuwa na mpango wala hatakuwa na mpango wa kulibadilisha. Ni yeye mwenyewe alisema pia kupitia kinywa cha nabii Isaya kwamba, agano lake hilo la Sabato ambalo ni agano la milele; litaendelea kutunzwa katika zama zote milele na milele hata huko peponi ambako kila mwislamu anatamani kufika. Sikia anavyosema;

“Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazozifanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na Sabato hata Sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana” (Isaya 66:22-23).

Rafiki yangu mpendwa, hakuna shaka yo yote kwamba katika vitabu vitakatifu vyote Mwenyezi Mungu anataja kuwa Sabato ndiyo hasa siku takatifu ya ibada ya kumheshimu na kumwabudu yeye peke yake. Tumeona katika somo hili kwamba, ni kweli kwamba vitabu vitakatifu vyote vinaeleza kwamba siku ya ijuma ni siku bora kabisa kwa sababu kuu mbili. Sababu ya kwanza ni kawamba Adamu baba yetu aliumbwa katika siku hiyo, na kwamba katika siku hiyo Adamu alisamehewa dhambi yake alipoomba msamaha. Hivyo, ni bora tukakumbuka siku ya ijumaa kama siku yetu ya kuzaliwa hapa ulimwenguni (siku ya kuumbwa kwetu). Lakini pia ni kheri tukiikumbuka kama siku ya mwanzo wa ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa msamaha wa dhambi ambao angewafanyia watu wake kupitia kumwagwa kwa damu. Ishara ya kumwagika kwa damu ya mnyama katika bustani ya Edeni ilikuwa ishara ya kumwagwa kwa damu ya thamani sana, ya Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu, damu ya Masihi Yesu. 

Hata hivyo pamoja na ubora huu wa siku ya ijumaa, Mwenyezi Mungu aliiteua, akaibariki na kuitakasa siku ya saba, siku ya Sabato kuwa siku ya ibada. Tumeona kwamba, kulingana na ushahidi wa historia, kuifanya ijumaa kuwa siku ya ibada, ni matamanio ya wanadamu tu, siyo maamrisho ya Mungu. Tumeona pia kwamba kutajwa kwa ijumaa ndani ya Qur’an ni kutokana na hali halisi ya mazingira ya wakati huo kwa watu wa Madina. Kwamba katika siku hiyo kulikuwa na soko kubwa katika mji wa Madina kiasi kwamba ilipelekea watu kuacha kuja katika ibada. Hii ndiyo ilivyo hata leo katika maeneo mengi ambapo kuna mnada katika siku za Jumamosi, Jumapili na Ijumaa; katika sehemu hizo, wengi huwa wanapuuzia ibada na kwenda zao sokoni kufanya biashara. Viongozi wengi wa dini katika maeneo hayo wana kibarua kigumu cha kupambana na waumini wao ili kuwafanya waje katika ibada. Hivi ndivyo ilikuwa kwa mtume Muhammad (s.a.w) wakati huo mpaka kupelekea kushuka kwa sura ya 62 (surat ul Jumua’). 

Je, kwa mujibu wa vitabu vitakatifu kuna siku maalumu ambayo Mwenyezi Mungu amemwagiza mwanadamu kufanya ibada?

Tumekwisha kuona kuwa siku ya ijumaa ni siku bora ambayo Adamu aliumbwa, na katika siku hiyo alisamehewa dhambi. Lakini hatujaona mahali iwapo Mwenyezi Mungu alimwagiza Adamu au mwanadamu yeyote kufanya ibada katika siku hiyo. Lakini pia tumeona kwamba Mwenyezi Mungu aliumba siku moja ya pekee sana, na kuipatia heshima kubwa kuliko siku nyingine zote. Hii ni kwa sababu siku hiyo imebarikiwa na kutakaswa, na tukaona kwamba maneno haya kubariki na kutakasa, ni maneno ya kidini, yanayohusikana na mambo ya ibada ya mwenyezi Mungu. Hivyo ni sahihi kusema kwamba katika siku ya saba au siku ya Sabato, ndiyo hasa siku ya kufanya ibada. Hii ni kutokana na maagizo ya Mwenyezi Mungu mwenyewe kama tulivyoona hapo juu kwamba, yeye ametuagiza kutofanya kazi siku hiyo (kutoka 20:8-11). Ni dhahiri kwamba ikiwa mwanadamu aliambiwa kutofanya kazi siku hiyo, bila shaka kuna jambo lingine ambalo Mungu alitaka mwanadamu afanye badala ya kufanya kazi. Tuangalie vitabu vitakatifu vinasema Mungu aliagiza jambo gani lifanyike katika siku ya sabato.

وَلَقَدْ‭ ‬عَلِمْتُمُ‭ ‬الَّذِينَ‭ ‬اعْتَدَوْا‭ ‬مِنكُمْ‭ ‬فِي‭ ‬السَّبْتِ‭ ‬فَقُلْنَا‭ ‬لَهُمْ‭ ‬كُونُوا‭ ‬قِرَدَةً‭ ‬خَاسِئِينَ

“Na kwa yakini mmekwisha yajua ya wale miongoni mwenu walioivunja Sabato, (siku ya mapumziko, Juma Mosi) na tukawaambia: Kuweni manyani wadhalilifu” (Qur’an Sura 2:65).

Shekhe Abdallah Saleh Farsy katika Tafsiri yake ya Qur’an, juu ya aya hii anasema kwamba;

“Mayahudi walikatazwa katika dini yao kufanya kazi siku ya jumamosi—wawemo ibadani tu. Lakini baadhi yao waliasi, ima kwa ujanja, au kinagaubaga (dhahiri bila ya kudanganya kwa kufanya ujanja wo wote). Basi Mwenyezi Mungu aliwaadhibu wote waliokhalifu, hata waliokhalifu kwa ujanjaujanja.”

Hapa Qur’an inataja wazi kwamba siku ya Sabato (jumamosi) ilifanywa kuwa siku ya ibada tu. Ni tamko la dhahiri kabisa nililolionyesha ndani ya Qur’an kwamba siku ya sabato ilikuwa siku ya ibada tangu zamani za wana wa Israeli. Je, Biblia nayo inakubaliana na Qur’an kwamba siku ya Sabato (jumamosi) ni siku ya ibada?

“Mtafanya kazi siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa. Kusanyiko takatifu; msifanye kazi ya namna yo yote; ni Sabato kwa Bwana katika makao yenu.” (Walawi 23:3).

Mwenyezi Mungu anasema kwamba, siku ya sabato ni kusanyiko takatifu, hili kusanyiko takatifu ni kusanyiko la ibada. Hivyo tunaona kwamba, kama ilivyosema Qur’an, siku ya Sabato ni siku ya kuwemo ibadani tu. Katika kitabu cha Isaya Mwenyezi Mungu anazidi kusisitiza kwamba siku ya Sabato ni siku ya kufanya ibada na sala. Tunasoma;

“Kama ukigeuza mguu wako usiihalifu sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita Sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya Bwana yenye heshima; ukiitukuza kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe; ndipo utakapojifurahisha katika Bwana…”.

“Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake; kila aishikaye Sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu; nitawaleta hao nao katika mlima wangu mtakatifu na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu yangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote” (Isaya 58:13, Isaya 56:6-7).

Tunaona katika aya hizi kwamba, Sabato imehusishwa na sala, pamoja na nyumba ya sala. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akasema siku ya Sabato, ni kusanyiko takatifu, watu wa Mungu wawemo ibadani tu. Siyo kufanya shughuli zingine zo zote. Katika siku hiyo Mwenyezi Mungu amesema, “usifanye kazi yo yote”. Lakini kama tulivyoona ndani ya Qur’an wapo watu ambao walikuwa na kiburi na kufanya ujanja ujanja kuihalifu Sabato ya Bwana. Mungu aliwalaani wakawa nyani wadhalilifu. Bila shaka mimi na wewe tusingependa kuwa nyani dhalilifu kwa kuvunja taadhima ya Sabato. Tunaona Mwenyezi Mungu hata ndani ya Biblia aliwakasirikia na kuwaambia;

“Tena wamenitenda haya; wamepatia unajisi mahali pangu patakatifu, siku ile ile, nao wamezitangua sabato zangu, Umevidharau vitu vyangu vitakatifu, umezitia unajisi Sabato zangu…ndipo niliposema, nitamwaga hasira yangu jangwani ili niwaangamize….” (Ezekieli 23:38; Ezekiel 22:8; Ezekiel 20:13).

Rafiki yangu mpendwa, hakuna shaka yo yote kwamba katika vitabu vitakatifu vyote Mwenyezi Mungu anataja kuwa Sabato ndiyo hasa siku takatifu ya ibada ya kumheshimu na kumwabudu yeye peke yake. Tumeona katika somo hili kwamba, ni kweli kwamba vitabu vitakatifu vyote vinaeleza kwamba siku ya ijuma ni siku bora kabisa kwa sababu kuu mbili. Sababu ya kwanza ni kawamba Adamu baba yetu aliumbwa katika siku hiyo, na kwamba katika siku hiyo Adamu alisamehewa dhambi yake alipoomba msamaha. Hivyo, ni bora tukakumbuka siku ya ijumaa kama siku yetu ya kuzaliwa hapa ulimwenguni (siku ya kuumbwa kwetu). Lakini pia ni kheri tukiikumbuka kama siku ya mwanzo wa ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa msamaha wa dhambi ambao angewafanyia watu wake kupitia kumwagwa kwa damu. Ishara ya kumwagika kwa damu ya mnyama katika bustani ya Edeni ilikuwa ishara ya kumwagwa kwa damu ya thamani sana, ya Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu, damu ya Masihi Yesu. 

Hata hivyo pamoja na ubora huu wa siku ya ijumaa, Mwenyezi Mungu aliiteua, akaibariki na kuitakasa siku ya saba, siku ya Sabato kuwa siku ya ibada. Tumeona kwamba, kulingana na ushahidi wa historia, kuifanya ijumaa kuwa siku ya ibada, ni matamanio ya wanadamu tu, siyo maamrisho ya Mungu. Tumeona pia kwamba kutajwa kwa ijumaa ndani ya Qur’an ni kutokana na hali halisi ya mazingira ya wakati huo kwa watu wa Madina. Kwamba katika siku hiyo kulikuwa na soko kubwa katika mji wa Madina kiasi kwamba ilipelekea watu kuacha kuja katika ibada. Hii ndiyo ilivyo hata leo katika maeneo mengi ambapo kuna mnada katika siku za Jumamosi, Jumapili na Ijumaa; katika sehemu hizo, wengi huwa wanapuuzia ibada na kwenda zao sokoni kufanya biashara. Viongozi wengi wa dini katika maeneo hayo wana kibarua kigumu cha kupambana na waumini wao ili kuwafanya waje katika ibada. Hivi ndivyo ilikuwa kwa mtume Muhammad (s.a.w) wakati huo mpaka kupelekea kushuka kwa sura ya 62 (surat ul Jumua’). Kwa nini rafiki yangu usiamue sasa kuanza kufanya ibada na kupumzika katika siku aliyoamrisha Mwenyezi Mungu watu wake kufanya ibada? Kwa nini usiichukulie sabato kuwa takatifu yenye heshima kwa kutozifuata njia zako? Kwa nini usijiunge na kundi kubwa la watu walioamua kumtii Mwenyezi Mungu na kushika maamrisho yake ili kwamba waweze kutambulikana kwa ishara hiyo kwamba wao ni watu wa Mwenyezi Mungu kweli kweli? Ni matumaini yangu kwamba Mwenyezi Mungu atakuongoza kufanya uamuzi sahihi kwa ajili ya uzima wako wa milele. Na ikiwa ni mapenzi yako watafute watu ambao wanashikilia msimamo huu wa kimaandiko, ambatana nao na kama utahitaji kujua zaidi watakufundisha. Mwenyezi Mungu akubariki sana unapofanya maamuzi haya ya hekima.

 

 

 

 

 

 

 



Related Information

Isemavyo Qur'an Kitabu kisichokuwa na shaka Nabii Isa ni nani hasa Nabii Isa: Kufa na kufufuliwa kwake