Vitabu vitakatifu vyote vinatuagiza kuamini mambo yafuatayo.
Tunasoma katika Qur'an kwamba.
ءَامَنَ ٱلرَّسُولُ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِۦ وَٱلْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَمَلَـٰٓئِكَتِهِۦ وَكُتُبِهِۦ وَرُسُلِهِۦ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِۦ ۚ وَقَالُوا۟ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ ٱلْمَصِيرُ
"Mtume ameanini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waislam vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, haatutafautishi baina ya yeyote katika mitume wake, na (Waumini) husema: Tumesikia na tumetii. Tunakutaka maghufira Mola Mlezi wetu! Na maregeo ni kwako.
Katika Biblia pia tunasoma kwamba;
"...mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndiyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa." (2Nyakati 20:20)
Katika ukrasa huu utajifunza mambo makuu haya ya Imani. Bwana akubariki sana.