Mwanzo wa Utume wa Paulo;

Katika Hesabu 12:6
Mwenyezi Mungu anaeleza namna mitume na Manabii wanavyopata Wahyi kutoka kwa Mungu:

"Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwepo nabii kati yenu, mimi Bwana nitajifunua kwake katika maono, nitasema naye katika ndoto..."

Je sifa hii ya kuletewa Wahyi Paulo alikuwa nayo?
Tunasoma katika Matendo. 16:9
“Wakati wa usiku Paulo akaona maono…”

Je Mungu alieleza kuwa Paulo alitumwa kwa watu gani?
Matendo. 9:15

“Lakini Bwana akamwambia Anania…Mtu huyu ni chombo changu kiteule nilichokichagua apate kulichukua jina langu kwa watu Mataifa na wafalme wao na mbele ya watu wa Israeli.”

Matendo 13:2
“Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema “Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi ile maalumu niliyowaitia”

Je Paulo Mwenyewe anajishuhudia vipi kuhusu utume wake?
Wagalatia 1:1
“Paulo, mtume, si mtume wa wanadamu aliyetumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo na Mungu Baba aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu”

Wakolsosai 1:1
“Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na ya Kristo Yesu tumaini letu.”

Hapa Paulo anatusaidia kujibu swali la Mada yetu, anasema ni “Mtume wa Mungu”

Bada ya kuangalia uthibitisho juu ya utume wa Paulo ndani ya Biblia Takatifu, hebu tuigeukie Quran tukufu ili kupata uthibitisho mwingine.

UTUME WA PAULO KWA MUJIBU WA QURANI TUKUFU

Kwa kuanza naomba niwakumbushe Waislam kwambu uislamu una sifa zifuatazo. (swifat ul I'iman mufaswalu)

1. Imani juu ya Mungu.

2. Imani Juu ya Malaika wa Mwenyezi Mungu.

3. Imani juu ya Vitabu vya Mwenyezi Mungu

4. Imani juu ya Mitume wa Mwenyezi Mungu

5. Imani juu ya Kheri na Shari za Mwenyezi Mungu.

6. Imani juu ya Siku ya Mwisho.

Kwa mujibu wa Mada hii. Nitajikita juu ya Imani juu ya Mitume.

Waislamu wanaamini kwamba, wapo Mitume wapatao 124,000. Kati ya hao. ni 25 tu ndiyo ambao mtume Muhammad (S. A. W) aliweza kupewa habari zake. kama tunavyosoma.

وَرُسُلًا قَدْ قَصَصْنَـٰهُمْ عَلَيْكَ مِن قَبْلُ وَرُسُلًا لَّمْ نَقْصُصْهُمْ عَلَيْكَ ۚ وَكَلَّمَ ٱللَّهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا


Na Mitume tulio kwisha kukuhadithia kabla yake, na Mitume wengine hatukukuhadithia. Na Mwenyezi Mungu alinena na Musa kwa maneno.( AN-NISAAI 4:164 )

Hii inamaana kwamba Muhamad alifahamu kidogo sana kuhusu habari za mitume. yaani kama ni asilimia ni 0.0002 ya uelewa wake juu ya mitume. na huo ndio uelewa wa waislamu wote linapokuja swala la mitume. Hata hivyo. Allah s.w alikwisha kumwelekeza mtume mahala pa kupata nuru zaidi aliposema.

فَإِن كُنتَ فِى شَكٍّ مِّمَّآ أَنزَلْنَآ إِلَيْكَ فَسْـَٔلِ ٱلَّذِينَ يَقْرَءُونَ ٱلْكِتَـٰبَ مِن قَبْلِكَ ۚ لَقَدْ جَآءَكَ ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلْمُمْتَرِينَ


Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia Haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wenye shaka. ((YUNUS 10: 94)

Hivyo kwa habari za mitume, karibia mitume wote aliosimuliwa muhammad wamo kwenye Biblia. Basi kama tulivyoona sehemu ya kwanza ya mada yetu leo twawagabarisha waislamu juu ya utume wa Paulo.

Hata hivyo ukisoma Quran kwa uangalifu utagundua kuwa Habari za Paulo zimeelezwa vizuri humo.

Chunguza aya hii.
Na wapigie mfano wa wakaazi wa mji walipo wafikia walio tumwa.
Tulipo watumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu. Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwenu.
( (YA-SIN 36:13-14))

Aya hii inaeleza kisa cha WAJUMBE WA MWENYEZI MUNGU.
Wafasiri na wanazuoni mfano Shekhe Bar wani, Yusufu Ali wamefasiri aya hii na kusema mji huo walikotumwa wajumbe ni ANTIOKIA.

Ibin Kathir katika tafsir yake anasema wajumbe hao ni Yohana, Simoni na Paulo.

Na hapa namnukuru ibn Kathir.

قال ابن جرير عن وهب بن سلمان عن شعيب الجبائي قال كان اسم الرسولين الأولين شمعون ويوحنا واسم الثالث بولص والقرية انطاكية  فقالوا » أي لأهل تلك القرية « إنا إليكم مرسلون » أي من ربكم الذي خلقكم يأمركم بعبادته وحده لاشريك له قاله أبو العالية وزعم قتادة أنهم كانوا رسل المسيح عليه السلام إلى أهل انطاكية « قالوا ما أنتم إلا بشر مثلنا » أي فكيف أوحي إليكم وأنتم بشر ونحن بشر فلم لا أوحي إلينا مثلكم ولو كنتم رسلا لكنتم ملائكة وهذه شبهة كثير من الأمم المكذبة كما أخبر الله تعالى عنهم في قوله عز وجل « ذلك بأنه كانت تأتيهم رسلهم بالبينات فقالوا أبشر يهدوننا »

Imesimuliwa na Ibn Jurayj kutoka kwa Wahb bin Sulayman, imepokelewa na Shu`ayb Al-Jaba'i, "Majina ya wajumbe wawili wa waliotumwa mwanzo ni Simoni na Yohana na jina la wa tatu ni Paulo. Na mji huo ulikuwa Antiokia” , and the city was Antioch. Na wakasema (kwa watu wa mji huo) “hakika sisi tumetumwa kwenu kama wajumbe”, hii ina maanisha “Wajumbe kutoka kwa Allah aliyewaumba nyinyi na anayewaamrisha mumwabudu yeye peke yake na msimfanyie washirika.” Qatada amesema walikuwa ni wajumbe wa Masihi Isa bin Maryam (a.s) waliotumwa kwa watu wa Antiokia. Wakasema “Ninyi ni wanadamu kama sisi…ni kwa vipi munaweza kupokea ufunuo wakati nyie ni wanadamu na sisi tu wanadamu kama nyie, kwanini sisi hatupokei ufunuo kama nyie?” hivi ndivyo ilivyokuwa kwa watu wa mataifa mengine walivyosema ‘hatuamini’, kama vile Allah anavyotuambia katika sura ya 64:6 , “Hayo ni kwa kuwa walikuwa wakiwajia mitume wao kwa hoja zilizo wazi, nao wakasema: Hivyo binadamu ndiyo atuongoe? Basi wakakufuru na wakageuka upande. Mwenyezi Mungu akawa hana haja nao…”

Imamu Twabariy pia katika kitabu chake cha Historia, Tarekhe Twabariy anasema.

حدثني الحارث، قال: حدثنا محمد بن سعد، قال: أخبرنا هشام، عن أبيه، عن أبي صالح، عن ابن عباس، قال: كان بين موسى بن عمران وعيسى بن مريم الف سنه وتسعمائة سنة، ولم يكن بينهما فترة، وإنه أرسل بينهما ألف نبي من بني إسرائيل، سوى من أرسل من غيرهم، وكان بين ميلاد عيسى والنبي خمسمائة وتسع وستون سنة، بعث في أولها ثلاثة أنبياء، وهو قوله: «إذ أرسلنا إليهم اثنين فكذبوهما فعززنا بثالث» ، والذي عزز به شمعون، وكان من الحواريين، وكانت الفترة التي لم يبعث الله فيها رسولا أربعمائة وأربعا وثلاثين سنة، وإن عيسى حين رفع كان ابن اثنتين وثلاثين سنة وستة أشهر، وكانت نبوته ثلاثين شهرا، وإن الله رفعه بجسده، وإنه حي الآن.

Amesimulia Haarath, amesema: Imesimuliwa na Muhammad bin Sa’ad, amesema: ametuhabarisha Hishaam, kutoka kwa babaye kutoka kwa Abiy Swaalih, kutoka kwa ibn Abbas, amesema: kulikuwa na miaka elfu moja na miatisa kati ya Musa mwana wa Imrani na Isa, kwa kipi hicho manabii elfu moja walitumwa kwa wana wa Israeli. Na kulikuwa na miaka mia tano na sitini na tisa kati ya kuzaliwa kwa Isa na Nabii (Muhammad), katika kipindi cha awali cha muda huu, walitumwa mitume watatu. Na hii ni kutokana na kauli yeke mwenyezi Mungu {{Tulipowatuma wawili, wakawakadhibisha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu…}}, na waliyezidishiwa ni Simoni, naye alikuwa miongoni mwa wanafunzi. Na kipindi ambacho mwenyezi Mungu hakutuma mitume kilikuwa miaka mianne na thalathini na nne. Na kipindi alipoinuliwa juu Nabii Isa alikuwa na umri wa miaka thelathini na mbili na miezi sita. Na kipindi cha unabii wake kilikuwa miezi thelathini. Na Mwenyezi Mungu alimnyanyua akiwa na mwili wake kama ulivyo, na hakika yeye yuko hai hata sasa.”

Hivyo kwa mujibu wa Sura ya 36:14 ndani ya Qur’an tukufu ni wazi kwamba, kabla ya kuja mtume Muhammad, wanachuoni wa kiislam wanaamini kwamba Mwenyezi Mungu alituma manabii watatu, na mmoja wa hao ni Mtume Paulo. Vinginevyo ikiwa wasilam wa sasa watalifanyia ukaidi jambo hili, watakuwa na wajibu wa kueleza umati wa waumini wao kwamba ni mitume gani waliokusudiwa katika aya hiyo?

Hivyo twaona kuwa hoja ya kumkataa Paulo ni uzushi wa hivi karibuni. Waislamu, wasomi na Maulamaa wa kale hawakuwa na hoja hii ya kumkataa Paulo.

UTUME WA PAULO KWA MUJIBU WA WANACHUONI WA AWALI WA KIISLAMU.

Baada ya Kuona Ushahidi wa vitabu vitakatifu juu ya utume wa mtume Paulo. Sasa tugeukie hadith za mtume Muhammad. na kwa nini tugeukie hadithi? Ni kwa ushauri unaotolewa na Allah s.w ndani ya Quran yenyewe.

[ AN-NISAAI - 59 ]
Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.

Katika kitabu kiitwacho SIRAT NABAWIYA. Kilichoandikwa na Ibn Hisham, aliyekuwa mwanafunzi wa ibn Ishak. Katika juzu ya 4 ya kitabu hicho uk 140 tunakuta Muhammad anaorodhesha majina ya Wanafunzi wa Yesu. na anawagawa katika mafungu 2. la kwanza ni wale waliomfuata wakati wa uhai wake na wale waliomfuata baada yakuwa amepaa juu. Muhammad anaeleza kila mmoja wa wanafunzi hao na mahala walikotumwa, kuhusu Paulo anaeleza kuwa Yeye alitumwa Rumi.

Na hapa namnukuru ibn Hisham.

*أسماء رسل عيسى عليه السلام*

أسماء رسل عيسى عليه السلام
قال ابن إسحاق ‏:‏ وكان من بعث عيسى بن مريم عليه السلام من الحواريين والأتباع ، الذين كانوا بعدهم في الأرض ‏:‏ بطرس الحواري ، ومعه بولس ، وكان بولس من الأتباع ، ولم يكن من الحواريين ، إلى رومية ، وأندرائس ومنتا إلى الأرض التي يأكل أهلها الناس ، وتوماس ، إلى أرض بايل من أرض المشرق ، وفيلبس إلى أرض قرطاجنة ، وهي أفريقية ؛ ويحنس إلى أفسوس ، قرية الفتية أصحاب الكهف ؛ ويعقوبس إلى أوراشلم ، وهي إيلياء قرية بيت المقدس ، وابن ثلماء إلى الأعرابية ، وهي أرض الحجاز ؛ وسيمن إلى أرض البربر ، ويهوذا ، ولم يكن من الحواريين ، جعل مكان يودس ‏.

(Tazama pia, Tarekhe Twabariy uk 600)‏

Majina ya Mitume wa Yesu Masihi:

“Amesema ibh Is-hak: walikuwa mionguni mwa wanafunzi wa Yesu (amani iwe juu yake) wale waliomfuata wale waliokuwa baada yake duniani: Petro Mwanafunzi wa Yesu, na pamoja naye alikuwepo Paulo miongoni mwa wafuasi, Paulo hakuwa miongoni mwa wale wanafunzi wa Yesu. Naye (Paulo) alitumwa Rumi. Na Andrea naye alitumwa katika nchi ambayo wakazi wake wanakula watu. Na Tomaso alitumwa katika nchi ya Babeli katika nchi za mashariki. Na Philipo alitumwa katika nchi pande za Afrika, na Yohana alitumwa Efeso na Yakobo alitumwa Yerusalemu na Batholomeo alitumwa Uarabuni katika nchi ya Hijaz. Na Simoni alitumwa Baribari.”

Yashangaza kuona kuwa licha ya ushahidi mkubwa namna hii waislamu wa leo (hasa wanaharakati) wameamua kufumbia macho ukweli huu na kuanza kudanganya watu. ama kwa maksudi ama kwakutokujua. SWALI NI HILI. wanafanya hivyo kwa faida ya nani?

Rafiki yangu mwislamu, napenda kukutahadharisha kwamba, shetani ni mjanja, siku zote atakuja kwa hila akiwatukia waalimu wa uongo, wengine watakuja kana kwamba ni watetezi wa dini kumbe ndiyo waharibifu wakubwa wa dini.

Allah s.w anasema ndani ya Quran kuwaambia waislamu
Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake. (AL - BAQARA 2:136)

Unaona kwamba Allah s.w amewaagiza waislam siyo tu kuamini wale kitume 25 waliotajwa ndani ya Quran lakini pia wanapaswa kuamini w aliyoteremshiwa wajukuu wa Yakobo, PAULO PIA NI MJUKUU WA manabii YAKOBO. Lakini siyo hivyo tu, Allah s.w amewataka manabii waislamu kuamini walioteremshiwa "manabii wengine". PAULO PIA NI MIONGONI MWA MANABII WENGINE.

Hivyo kumpinga Paulo ni kuipinga imani, kupinga Quran na Mwinsho kumpinga Allah mwenyewe. NA HUU NDIO UKAFIRI ULIOKITHIRI.

Je kuha hadithi yoyote ya Mtume mahali ambapo, Mtume aliwatahadharisha masahaba zake au Waislamu kwa ujumla juu ya Mafundisho ya Paulo?

Hapana, badala yake tunaona Muhammad yeye mwnyewe alinukuru mafundisho ya Paulo na akiuita ni ujembe kutoka kwa Mwenyezi Mungu‏

“Imesimuliwa na Abu Huraira, Mjumbe wa Allah (s.a.w) alisema; Mwenyezi Mungu kasema, ‘Nimewaandalia waja wangu ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio halijawahi kusikia wala moyo wa mwanadamu hauwezi kuyafikiri”

Hivyo twaona kuwa hoja ya kukataa utume wa Paulo hainamsingi wa mafundisho ya vitabu vitakatifu, ni upotoshaji wa waalimu wa dini wanaotafuta masilahi yao binafsi. Hivyo ninakusihi rafiki yangu usikubari kudanganywa na watu ambao wamekusudia kuwapoteza watu au wanafanya hivyo bila kujua. Lichukue Neno la Mwenyezi Mungu lote na ulisome kwa uzima wako wa bilele. Unaweza kuwasiliana nasi pia kupitia mawasiliano  yaliyo wekwa hapa, ili kupata Biblia yako bure kama zawadi kwa kuendelea kutufuatilia ikiwa ni pamoja na masomo mengine ya Biblia.

 



Related Information

Imani Je Shetani alitoka wapi? Mwongozo kwa wamchao mwenyezi Mungu Waja wema watairithi nchi